Fashion

Saturday, February 22, 2014

WAYNE ROONEY AULA MAN UTD,NI BAADA YA KUSAINI MKATABA MPYA!!....

MSHAMBULIAJI Wayne Rooney,amesaini mkataba wake mpya katika klabu ya Manchester Utd itakayomhakikishia kuwa hapo old Trafford kwa miaka mitano.Wayne Rooney atalipwa Pauni laki 300,000kwa wiki inayofanya awe mchezaji anayelipwa hela nyingi duniani.


Wayne Rooney
Rooney ambaye alitaka kuondoka mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kutofautiana na aliyekuwa kocha wa timu hiyo Sir Alex Ferguson,aliwaambia mashabiki wake katika ukurasa wake wa facebook kwamba"imekuwa siku nzuri sana ,mimi kusaini mkataba mpya na klabu hii"


Ed Woodward,Wayne Rooney and David Moyes
Rooney amemshukuru sana Kocha wake Moyes,ambaye amesema wamekuwa na mahusiano mazuri toka Moyes atue Old Trafford.

Hongera zako Rooney,tunakutakia kila la kheri!!

No comments:

Post a Comment